Jumatano , 19th Feb , 2025

Baada ya La Liga, UEFA sasa pia imechukua hatua kwa kumsimamisha mwamuzi Munuera Montero kuchezesha mashindano ya Ulaya hadi itakapotangazwa tena.

Jude Bellingham akihamaki baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu na refa Jose Luis Munuera Montero

Montero anatuhumiwa kumtoa nje ya Uwanja Jude Bellingham kwa Kadi nyekundu kimakosa katika mchezo wa La Liga ambao ulitamatika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Rayo Vallecano baada ya kupishana lugha Jumamosi Februari 15.

Hatua hii ya UEFA imekuja baada ya Klabu ya Real Madrid kulalamika kutoridhishwa na waamuzi wa Ligi ya Uhispania (La Liga) baada ya matukio ya kuonewa katika michezo kadhaa.

Pia, Madrid wametishia kuhama ligi ya La Liga endapo hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwa upande wa waamuzi. Ligi wanapozanga kuhamia ni Lihi ya Nchini Italia (Seria A), Ligi ya Nchini Ujerumani (Bundasliga) na Ligi ya Nchini Ufaransa (Ligue 1)