Ijumaa , 14th Feb , 2025

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amesema kuwa Kyiv haitakubali makubaliano yoyote ya amani yaliyofikiwa na Urusi na Marekani bila ushiriki wake.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amesema kuwa Kyiv haitakubali makubaliano yoyote ya amani yaliyofikiwa na Urusi na Marekani bila ushiriki wake.

Hii inajiri baada ya Donald Trump kuzungumza na Vladimir Putin Jumatano kabla ya kutangaza kuwa walikubaliana kuanza mazungumzo ya kumaliza vita vya Ukraine “mara moja”.

Zelensky alifichua kuwa alimueleza Trump kuwa kipaumbele kwa nchi yake ni ''hakikisho la usalama'',akilitaja hilo litakuwepo Marekani ikiwasaidia.

Awali, Trump alisema kuna “uwezekano mzuri” wa kumaliza vita hivyo.

Inasemekana baadhi ya Waukraine wanahofia kuwa Putin huenda akajaribu kumlipa Trump ili kupata manufaa, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Rustem Umerov, akiwahakikishia washirika wa NATO kuwa nchi yao ni “imara, ina uwezo na itatekeleza”.