![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2025/02/09/SAMM.jpg?itok=v38HbnTM×tamp=1739120709)
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira
Amesema CCM ina mipango mizuri kuhakikisha vijana hao wanatumia nguvu zao kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kujikwamua dhidi ya umasikini.
Wasira aliyasema hayo alipokuwa akizindua ofisi ya CCM Kata ya Nyakonga wilayani Tarime, Mkoa wa Mara.
"Nataka niwaambie wananchi wa Tarime CHADEMA wakitaka kufanya fujo mahali popote wanakuja kuchukua vijana Tarime wanapelekwa kufanya fujo kama majeshi ya kukodi, wakitaka kufanya fujo Mbeya wanakuja, Tarime, wakitaka kufanya fujo sehemu Tarime," amesema Wasira
"Tunawaambia vijana wa Tarime wana mvua wana jua na Tarime panalimika, kila kitu kinaota tuwasaidie vijana wa Tarime watumie fursa zilizopo, tunawaambia CHADEMA muache kuja kuchukua vijana Tarime, sisi sio eneo la mapambano, vijana wetu sio wa kukodisha kwenda katika mapambano, nasema kama mzee wa Tarime waache kuja kuchukua vijana wa Tarime,"
Wasira amewataka vijana wasikubali kuchukuliwa na kutumika katika vurugu kwa kuwa wakienda huko hupigwa, kuumizwa na hata kupata ulemavu kisha kurudishwa Tarime wakiwa na hali mbaya.