"Sisi kama Serikali tumeshachukua hatua kali kupitia TCRA na utakuwa pia shahidi kuwa wimbi la meseji limepungua kwa kiasi fulani, ilikuwa balaa zaidi ya ambavyo ipo sasa TCRA inaendelea na namna mbali mbali ya kuhakikisha inadhibiti hizi laini ambazo zimepatikana kwa njia zisizo sahihi kwahiyo kama serikali ishachukua hatua na kazi inaendelea"
"Na mkakati wa kuwapunguza hawa freelancers ambao wanapita huko kurahisisha kuwafikia wananchi, lengo lilikuwa zuri hawa vijana waweze kuwafikia kule wananchi kuwapunguzia ugumu wa upatikanaji wa laini lakini matumizi yamekwenda kuwa mabaya lakini tayari pia tumepumguza sana namna ya hawa freelancers kuzagaa huko kwenye jamii lakini vile vile tumehakikisha kuendelea kuwa na udhibiti kuona kwamba laini za simu zitapatikana maeneo maalumu"
Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi akijibu swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga aliyeuliza kuhusu ulaghai wa upatikanaji wa laini na vitendo vya utapeli mitandaoni ikiwemo na mawakala wanaosajli laini leo Januari 31 bungeni jijini Dodoma.