Jennifer Mbuya, Meneja Mahusiano Airtel
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa simu hiyo ya A80 Meneja Uhusiano wa Airtel nchini, Jennifer Mbuya ameeleza sababu kubwa ya airtel kushirikiana na itel ni kupunguza mgawanyiko wa kidijitali nchini kupitia teknolojia suluhishi kwa bei nafuu.
"Ushirikiano wetu na itel utaongeza matumizi ya simu kwa watumiaji wa Airtel kote nchini kwa kuchanganya vipengele vya kisasa vya itel na mtandao bora wa Airtel wenye kasi zaidi. Ushirikiano huu unaonyesha jinsi unavyojitolea katika kurahisisha maisha ya wateja wetu kupitia bidhaa za kibunifu", Jennifer Mbuya, Meneja Mahusiano Airtel
Akizungumza kwa niaba ya itel, Meneja masoko wa kampuni hiyo Sophia Msafiri ameeleza namna ambavyo ushirikiano na airtel utachagiza maendeleo ya kidijitali nchini na kurahisisha huduma ya mawasiliano kwa jamii kubwa ya Tanzania.
"Lengo kubwa ni kuhakikisha tunaifikia jamii kubwa ya Tanzania yenye uhitaji wa simu kwa gharama nafuu, ushirikiano wetu na airtel itakuwa chachu ya kukamilisha ndoto za wengi kumiliki simu yenye uwezo mkubwa na kasi ya mtandao wa Airtel zaidi", Sophia Msafiri, Meneja Masoko Itel
Kwa upande wa mtumiaji wa simu ya Airtel iliyounganishwa na huduma ya mtandao wa Airtel ameeleza faida ya kutumia simu ya A80 ikiwemo kudumu kwa chaji kwa kipindi kirefu na uimara wa simu hiyo.
"Simu za Itel zenye ofa ya Airtel ni simu imara ambazo ofa yake ni kubwa zaidi, inakaa na chaji kwa muda mrefu na uimara wake si sawa na simu nyengine", Yona Samwel, Mteja wa Airtel
Airtel ni Kampuni ya mtandao wa simu yenye kasi zaidi nchini, imejipambanua kwenye ubora na huduma nzuri kwa wateja, ushirikiano kati ya Airtel na Itel utarahisisha ukuaji wa kidijitali na teknolojia ya kisasa zaidi.