Jumanne , 17th Mar , 2015

Wahamiaji haramu raia wa Ethiopia wapatao 63 wamefikishwa katika mahakama ya Mkoa wa Dodoma leo kujibu shitaka linalowakabili la kuingia nchini kinyume cha sheria.

Wahamiaji kutoka Ethopia wakipata kifungua kinywa.

Akisoma mashtaka mbele ya hakimu Mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Dodoma, Rebecca Mbilu mwendesha mashtaka wa serikali, Lina Magoma alisema Waethiopia hao waliingia nchini kinyume cha sheria namba 31 kifungu cha 1(1) na (2) cha sheria ya uhamiaji cha mwaka 2002.

Hata hivyo washtakiwa hao walikubali kosa kwa kusaidiwa na mmoja wao ambaye alikuwa anajua kiingereza na kuwatafsiria kwa lugha ya Kihabeshi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 20 mwaka huu ambapo itasikilizwa tena na washtakiwa hao walirejeshwa rumande kwa kuwa kesi yao haina dhamana.