Wakizungumza na waandishi wa habari ndugu wa marehemu wamesema tukio hilo lilitokea Oktoba 30 mwaka 2024 majira ya saa 6:00 usiku katika kijiji cha Mwamashiki ambapo inadaiwa kijana huyo alivamiwa wakati amelala na mwanamke anayesadikika kuwa ni mke wa mwanaume anayedaiwa kufanya uvamizi huo.
"Yule Baba alikuja kwa namna ya kugonga mlango akamuita mke wake baada ya kumuita mke wake mwanamke akamwambia yule wa ndani tumekutwa mume wangu amekuja baada ya hapo inasemekana kaka yangu akaamua kufanya maamuzi ya kupanda juu ya dari basi yule mama akafungua mlango yule mwanaume akaingia, baada ya kuingia yule baba akafunga ule mlango akaanza kumponda na mawe kule juu alipoanguka ndipo akaanza kumkatakata mapanga baada ya kumaliza kumkata kutazama vizuri akashangaa eeh kumbe nimemkata mapanga mtu ambaye sio niliyekuwa natarajia kuja kuua siyo mwenyewe akawa amepanda pikipiki haraka akaenda," amesema Dada wa marehemu
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita SACP Safia Jongo amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mtuhumiwa ni fundi wa kuchana mbao mwenye umri wa miaka 39 na tayari anashikiliwa na jeshi la polisi na wakati wowote atafikishwa mahakamani.