Alhamisi , 31st Oct , 2024

Mahakama Kuu nchini Kenya imeiondoa kesi ya kusitishwa kuteuliwa kwa Naibu Rais wa Kenya Profesa Kithure Kindiki, aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais William Ruto, mara baada ya bunge la seneti nchini humo kuridhia aliyekuwa akishika wadhifa huo Rigathi Gachagua aondolewe madarakani.

Profesa Kithure Kindiki

Jopo la majaji watatu wakiongozwa na Erick Ogolla, limesema limechukua uamuzi huo kwa kuzingatia kwamba Ofisi ya Naibu Rais haiwezi kuendelea kubaki bila kuwa na mtu na Profesa Kindiki ataapishwa hapo kesho.

Uamuzi huo sasa unaruhusu kuapishwa kwa Kithure Kindiki kama Naibu Rais wa Tatu wa Kenya na kwamba Gachagua anaweza kuukatia rufaa uamuzi huo.