Jumanne , 29th Oct , 2024

Klabu ya Sporting Lisbon imetoa tamko kuhusiana na klabu ya  Manchester United  kukubali  kulipa kiasi cha fedha  bilioni 17 za Kitanzania ili kuweza kupata huduma ya Kocha wao Ruben Amorim ambaye anahitajika na klabu hiyo ya Uingereza kuchukua nafasi ya Erik Ten Hag  waliyemfuta kazi jana

Ruud van Nistelrooy atakiongoza kikosi cha Mashetani Wekundu katika mchezo wa ligi siku ya kesho Jumatano dhidi ya Leicester City, huku klabu ikisubiri kumtambulisha Kocha mkuu muda wowote kuanzia siku ya  kesho. 

Klabu ya Sporting Lisbon imetoa tamko kuhusiana na klabu ya  Manchester United  kukubali  kulipa kiasi cha fedha  bilioni 17 za Kitanzania ili kuweza kupata huduma ya Kocha wao Ruben Amorim ambaye anahitajika na klabu hiyo ya Uingereza kuchukua nafasi ya Erik Ten Hag  waliyemfuta kazi jana Jumatatu.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo Mabingwa wa kihistoria  kombe la ligi kuu Uingereza EPL  zinasema Mkufunzi huyo anatarajiwa kuanza kibarua chake kipya kabla ya mchezo wa Man U dhidi ya Chelsea mchezo utakaochezwa kwenye dimba la Old Trafford siku ya Jumapili.

Ruud van Nistelrooy atakiongoza kikosi cha Mashetani Wekundu katika mchezo wa ligi siku ya kesho Jumatano dhidi ya Leicester City, huku klabu ikisubiri kumtambulisha Kocha mkuu muda wowote kuanzia siku ya  kesho. 

Amorim raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 39, anapewa kipaumbele na Mabosi wa United kutokana na kazi nzuri anayoifanya ndani ya Sporting Lisbon ambapo ameiongoza timu kushinda taji lake la kwanza baada ya miaka 19 kupita mbele ya FC Porto na Benfica.

Anatizamwa kama Mwalimu bora kwasasa kutokea Ureno baada ya Jose Mourinho na alihitajika na Vilabu vingi ikiwemo Liverpool ya Uingereza baada ya Jurgen Klopp kuondoka kabla hawajampata Arne Slot, Nyota huyo wa zamani wa Benfica alichagua kubaki Lisbon ili kuendelea kupata kujifnza zaidi maswala ya uongozi na amahisi sasa yupo tayari kuchukua majukumu ya kufundisha timu kubwa.

Kiungo huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno atakuwa Mkufunzi wa sita kuifundisha Manchester United baada ya Sir Alex Ferguson kustaafu mwaka 2013. Man United inashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa EPL baada ya kucheza michezo 9 ikishinda mitatu ikitoka sare miwili na kufungwa minne.

Klabu hiyo inayotumia uwanja wa Old Trafford haijashinda taji la ligi kuu Uingereza tangu mara ya mwisho hivyo msimu wa 2012-2013. Ujio wa Ruben Amorim unatizamwa kama mwanzo mpya, na Viongozi wake wanaimani kubwa kwa raia huyo wa Ureno kutokana na Walimu kutoka nchini hiyo kufanya vizuri EPL.

Nuno Espírito Santo,Marco Silva ni mfano mdogo wa Walimu kutoka Liga Portugal wanaofanya vizuri kwenye ligi ya Uingereza kutokana na aina ya mpira wanaofundisha kwenye vilabu vyao vya Nottingham Forest F.C. na Fulham F.C. pia wameonyesha jinsi gani imekua rahisi kwa Wachezaji na Makocha kutoka ligi hiyo kuzoea mazingira ya kufanya kazi Uingereza.

Ruben Amorim anatarajiwa kutangazwa muda wowote kwenye klabu ya Man United ili kuanza kazi ya kukifundisha kikosi chenye mchanganyiko wa Wachezaji wachanga na wenye uzoefu, kazi yake itakuwa ni kwenda kubadili wimbi la matokeo mabovu ya hivi karibuni baada ya kucheza michezo 8 ya mashindano yote na kufanikiwa  kushinda mchezo mmoja.