Jumatatu , 28th Oct , 2024

Stephen amewahi kushinda tuzo ya MVP mara mbili  amekuwa na historia ya kuumia kifundo cha mguu wake mara kwa mara   amefunga alama 18 huku Warriors ikipoteza mchezo wake wa kwanza wa NBA msimu huu.

Nyota wa Golden State Warriors Stephen Curry amepata majeraha timu yake ikipoteza dhidi ya Los Angeles Clippers kwa alama   112-104. Curry alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi ya kikapu nchini Marekani maarufu NBA dhidi ya Clippers mchezo uliochezwa jana Jumapili Oktoba 27, uwanja wa Chase Center.

Curry alionekana kuchechemea kwenye robo ya tatu ya mchezo  kutokana maumivu kwenye  kifundo chake cha mguu wake. Nyota huyo mwenye umrio wa miaka 36 alirejea uwanjani dakika ya nne katika robo tatu ya mchezo baada ya kupatiwa matibabu alishindwa kuendelea na mchezo na kusababisha kusindikizwa chumba cha kupatiwa huduma zaidi na  Gary Payton.

Stephen amewahi kushinda tuzo ya MVP mara mbili  amekuwa na historia ya kuumia kifundo cha mguu wake mara kwa mara   amefunga alama 18 huku Warriors ikipoteza mchezo wake wa kwanza wa NBA msimu huu.

Ivica Zubac na James Harden wote walifunga alama 23 kwenye ushindi huo wa Clippers.

Mchezo wa pili mfululizo Ivica Zubac raia wa Crotia amefanikiwa kuondoka na alama kwenye mchezo akiwa amefunga alama zaidi ya kumi na kufanya ribaundi zaidi ya kumi amefunga alama 23, amecheza ribaundi 17 akifanya usaidizi wa alama sita.

Kwengineko  Boston Celtics ilipata ushindi dhidi ya Detroit Pistons 124-118, Houston Rockets ilipoteza dhidi ya 109-106  San Antonio Spurs.

 Miami Heat ilishinda dhidi ya  Charlotte Hornets 114-106 baada ya kuzindua sanamu la aliyewahi kuwa mchezaji nyota kwenye ligi ya NBA Dwayne Wade.

Dwane Wade ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Heat  aliwahi kuiongoza timu hiyo  kushinda ubingwa wa ligi ya kikapu Marekani NBA mara tatu kipindi anakitumikia kikosi hiko.

Kuumia kwa Stephen Curry ni pengo kubwa kwa Golden State Warriors kutokana na ubora wake wa kufunga alama tatu pale anapopata nafasi ya kukiona kikapu kukosekana kwake kutaathiri jitihada za kikosi cha Kocha Steve Kerr.