Jumamosi , 26th Oct , 2024

Jeshi la polisi mkoani mwanza linamshikilia Dereva wa basi la abiria lenye namba za usajili T 622 EFG linalofanya safari zake mkoani mwanza kwenda Morogoro kwa kukutwa na leseni ya kuendesha pikipiki huku yeye ni dereva wa basi la abiria.

Akizungumza na wakati ukaguzi wa magari yanayofanya safari za usiku kutoka Jijini Mwanza kuelekea mikoa mingine Kamanda wa Jesho la polisi DCP Ramadhani ng’azi  amesema ukaguzi huo ni mwendelezo wa ukaguzi wa magari yasiyokidhi vigezo na masharti ya kubeba abiria ili kuokoa ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara.

“Huyu Sio dereva wa gari la abiria leseni yake ukomo wake ni kuendesha pikipiki. Na tunaendelea na operesheni ya ukaguzi wa magari yanayofanya safari za usiku na yaliyoanza safari zake za mwanza na Shinyanga na katika operesheni hii jumla ya magari yaliyokaguliwa ni mabasi 53, yaliyoandikiwa faini ni mabasi 15, madereva wasiokidhi vigezo 2.” Amesema DCP Ramadhani Ng’azi

Aidha abiria wameshukuru Jeshi la Polisi kwa kuendelea na ukaguzi wa mabasi na ili kuhakikisha wanasafiri salama na wameomba ukaguzi huo usiwe mwanzo wa safari tu hata mwisho wa safari hii itasaidia kuokoa maisha

“tunashukuru jeshi la polisi kwa kuendelea na operesheni hii inayofanyika na tunaomba zoezi hili liwe endelevu pale safari zinapoanza na hata linapo komea kwa kweli itatusaidia hata usalama wa maisha yetu.” Amesema Moja ya abiria