Alhamisi , 24th Oct , 2024

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha wanashirikiana na mamlaka ya mapato (TRA) kuhakikisha wanadhibiti uingiaji wa bidha za magendo katika mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema kumekuwa na njia nyingi zinazotumika kupitisha magendo kuingia na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinashirikiana na mamlaka ya mapato kujua vitu vinavyobebwa kwenye magari ya mizigo iingiayo ndani ya mkoa wa Dar es salaam wakati alipotembelea katika kituo cha polisi Mabwepande

“Sasahivi kuna wimbu kubwa sana la uingiaji wa bidhaa za magendo bidhaa za magendo hizii kwa mfano unakuta kuna mashua huko zinaleta mizigo simamieni vizuri pia kwa kushirikiana na mamlaka za mapato ili tuweze kujua wamebeba kitu gani.” Amesema Albert Chalamila

Aidha Mkuu wa Mkoa amesema hivi karibuni kumekamatwa madawa ya kulevya kwenye fukwe za kunduchi na mbweni na kameshna madawa ya kulevya na kuzitaja athari mbalimbali za madawa ya kulevya na kuvitaka vyombo vya usalama kuhakikisha vina dhibiti uingiaji wa madawa katika mkoa wa Dar es Salaam.

Sambamba na hilo  vyombo vya ulinzi na usalama vimetakiwa kuhakikisha vinahakikisha kunakuwa na ulizi na kusalama katika mkoa wa Dar es Salaama na endapo yeyote atabainika kutaka kuvuruga Amani basi achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.