Jumatano , 23rd Oct , 2024

Msanii Michael Adebayo Olayinka Maarufu kama Ruger kutoka nchini Nigeria amefunguka moja kati ya wasanii ambao angetamani kabisa kufanya nao wimbo kama wangelikuwa hai basi ni mfalme wa muziki wa rege duniani Robert Nesta Marley Maarufu kama Bob Marley

Pichani ni msanii Ruger na Bob Marley

Ruger ameyasema hayo akihojiwa na mwanamitandao huko nchini Nigeria ambapo aliulizwa kama angeweza kufanya kazi na msanii yoyote aliyehai na asiyehai angekuwa nani ambapo msanii Ruger alitaja jina la legend wa muziki Bob Marley kama msanii ambaye angetamani sana kufanya nae wimbo.

 Ruger pia amemtaja msanii Wizkid kama msanii maarufu zaidi mwenye namba yake,mbali na hilo ameutaja wimbo wake wa Wewe kama wimbo wake pendwa zaidi kwenye kuutumbuiza.

Msanii Ruger amezaliwa mwaka 1999 hivyo kwasasa ana umri wa miaka 25,alianza rasmi muziki mwaka 2021 akiwa chini ya recording label ya Jonzing huko lagos nchini Nigeria.