Jumatano , 16th Oct , 2024

Thomas Tuchel koch wa zamani wa Chelsea aliiongoza klabu ya The Blues kushinda kombe la klabu bingwa Ulaya pamoja na kombe la klabu bingwa Dunia msimu 2020-2021. Mafanikio hayo na timu hiyo ya Jiji la London yalimpa tuzo ya Kocha bora wa Ulaya na Dunia mwaka 2021.

Thomas Tuchel kocha wa zamani wa Chelsea ya England amesaini mkataba wa miezi 18 kuiongoza timu ya taifa ya England. Kikosi hicho mabingwa wa kombe la Dunia mwaka 1966 kilikua chini ya Kocha wa muda Lee Carsley baada ya aliyekua Mkufunzi mkuu wa timu hiyo Gareth Southgate kujiuzulu mwezi Julai 2024. Tuchel anakuwa Mwalimu wa tatu ambaye si raia wa Uingereza kuiongoza England baada ya Sven- Goran Eriksson na Fabio Capello. Mjerumani huyo aliyewahi kushinda tuzo ya Kocha bora Ulaya na Dunia mwaka 2021 atasaidiwa na Antony Barry aliyefanya naye kazi Chelsea na Bayern Munich.

Thomas Tuchel kocha wa zamani wa Chelsea ya England ametangwaza na FA ya nchi hiyo kuwa kocha wao mkuu baada ya Gareth Southgate kujiuzulu mwezi Julai 2024. Kikosi cha Three Lions ( Simba Watatu ) kipo chini ya uangalizi wa kocha wa muda Lee Carsley ambaye ataiongoza timu hiyo mpaka Disemba 31 2024.

Tuchel raia wa Ujerumani amesaini mkataba wa miezi kumi na nane na atasaidiwa na Antony Barry ambaye aleshawahi kufanya naye kazi Chelsea na Bayern Munich. Kwa pamoja Makocha hao wataanza majukumu yao mapya katika timu ya taifa ya England Januari 1, 2025.

Mjerumani huyo aliyewahi kushinda tuzo ya Kocha bora wa mwaka wa Ulaya na Dunia mwaka 2021 baada ya mafanikio aliyoyapata msimu wa 2020-2021. Alikiongoza kikosi cha The Blues kushinda makombe ya klabu bingwa Ulaya pamoja na ubingwa wa klabu bingwa Dunia mwaka 2021. Mkufunzi huyo anahistoria ya kushinda makombe akiwa na Borrusia Dortmund ya Ujerumani , PSG ya Ufaransa na Chelsea ya England.

Baada ya kujiuzulu kwa Gareth Southgate FA ya nchi ya nchi hiyo mabingwa wa kombe la Dunia mwaka 1966, ilianza mchakato wa kutafuta Kocha mpya ambapo majina mengi yalitajwa mpaka pale viongozi wa Shirikisho hilo la Soka lilipoona Tuchel ndiye anayefaa kuiongoza timu ya taifa lao. Mkufunzi huyo wa zamani wa timu Matajiri wa Jiji la Paris alisaini mkataba tangu Oktoba 8, 2024 kutangazwa kwake kumecheleweshwa sababu za kupisha timu ya taifa iliyokuwa inashiriki michezo ya ligi ya mataifa ya Ulaya.

Kocha huyo wa Dunia mwaka 2021 anakuwa kocha wa tatu asiye raia wa Uingereza kuiongoza timu ya taifa ya England baada ya Sven- Goran Eriksson na Muitaliano Fabio Capello.

Tuchel mwenye miaka 51, atakuwa na kazi ya kuwaongoza Wachezaji wenye vipaji vikubwa wa Three Lions kutwaa ubingwa wa mashindano makubwa baada ya kufika nusu fainali kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi, Fainali ya Kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka 2020 na 2024 ambapo kikosi hiko kilipoteza michezo yote ya fainali mbele ya timu za Italia na Hispania. England imetwaa ubingwa wa mwisho mkubwa kwa upande wa timu za taifa 1966 kombe la Dunia  fainali zilizofanyika kwenye  ardhi yao.