Ijumaa , 11th Oct , 2024

Mbunifu wa Mavazi Khadija Mwanamboka amesema kila mbunifu wa Tanzania ana ndoto ya kutaka kumvalisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu na Khadija Mwanamboka kushoto

Khadija Mwanamboka amefunguka hilo mbele akizindua Samia Fashion Festival ambayo ni  challenge inatoa fursa ya wabunifu kuandaa mavazi ambayo anaweza kuvaa Rais Samia.

"Kila mbunifu duniani anatamani kumvalisha Rais wa nchi yake, hata mimi natamani kumvalisha Rais Samia. hiko ni kitu kikubwa sana kwenye kazi ya Mbunifu" - amesema Khadija Mwanamboka