Jumanne , 8th Oct , 2024

Jamii imetakiwa kuonesha umuhimu wa usawa wa kijinsia kuanzia ngazi ya familia ili watoto wanapofika kwenye ngazi mbalimbali za Elimu wawe na uelewa mpana utakaowasaidia kuepukana na changamoto za ukatili.

Hayo yamesemwa na Naibu makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Wineaster Saria kwenye jukwaa la usawa wa kijinsia lililofanyika Leo jijini Dar es Salaam kuhusu namna bora ya kuunganisha usawa wa jinsia kwenye mabadiliko ya uchumi.

“Mtoto anapozaliwa lazima aoneshwe umuhimu wa usawa wa kijinsia ili hata anapoenda shuleni kufika mpaka chuo kikuu isiwe kitu kipya na hiyo itasaidia kupunguza changamoto zilizopo”, PROF. WINEASTER SARIA-Naibu …