Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua
Kulingana na wabunge wanaounga mkono hoja ya kumtimua bungeni, Gachagua ana hatia ya madai yote na wabunge hao wako tayari kuwasilisha ushahidi kuhalalisha hilo.
Matokeo ya mchakato wa ushiriki wa umma ambao uliendeshwa na Bunge la Kitaifa yanaonesha, asilimia 65.11 ya Wakenya walioshiriki katika zoezi hilo wanaunga mkono kuondolewa huku asilimia 33.80 wakipinga.
Ripoti hiyo ilisema jumla ya watu 224, 907 walishiriki zoezi hilo katika maeneo bunge 290, waliojumuisha Wakenya 10 walioko ughaibuni.
Ripoti hii wakati ikijadiliwa bungeni mapema leo, wabunge walitoa maoni tofauti kuhusu hoja ya kumuondoa madarakani, huku wengi wao wakiunga mkono hoja ya kumbandua Naibu Rais.