Jumanne , 8th Oct , 2024

Mbunge wa jimbo la makambako Deo Sanga amemtaka waziri wa elimu kuhakikisa anatekeleza ujenzi wa shule ya ufundi katika wilaya ya makambako ili kufundisha wanafunzi katika wilaya hiyo kwa eneo limeshatengwa na lipo tayari kwa ujenzi.

Mbunge wa Makangako Deo Sanga akizungumza na wananchi wa wilaya ya makambako

Deo sanga ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa wodi ya wagonjwa katika kituo cha afya Lyamkena kilichopo wilayani hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Elimu prof. Adolf Mkenda na kumtaka waziri kukamilisha ujengi wa shule ya ufundi kwani apo awali ujenzi wa chuo cha veta ulishindikana.

“Nilikuomba wakati nimekuja mimi mwenyewe ofisini kwako nikikuomba katika wilaya yetu ya makambako na eneo tumesha tenga tuna ekari 35 kutokana na sababu ambazo sitozitaja hapa sasa tunaomba utupatie fedha tujenge shule ya ufundi badala ya shule chuo cha veta kama tulivyo omba” amesema Deo Sanga

Aidha waziri wa elimu Prof. Adolf Mkenda amesema amepokea ombi hili ambalo analifanyia kazi kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ili wanafunzi wilayani waweze kunufaika na shule hizo za amali za ufundi.