Mh. Rosemary Senyamule, amempongeza Mbunge wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Anthony Mavunde kwa jitihada mbalimbali anazofanya katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Dodoma huku akieleza kuwa mitungi hiyo ni sehemu ya utunzaji mazingira kwa kutumia nishati mbadala ili kuepukana na matumizi ya kuni na mkaa lakini pia kupunguza muda wa kupika.
“Asante sana Mhe. Mbunge kwa kutuletea mitungi hiyo rafiki kwa mazingira, sasa tutapika kwa wakati mfupi, tunakushukuru kwa kuwajali wananchi kata zote za Jimbo la Dodoma pamoja na taasisi mbalimbali za umma. Nendeni mkatumie mitungi hiyo ya kisasa, kati ya wabunge wanaofanya kazi vizuri, Mavunde yumo, Mavunde ni kijana mchapakazi na msikivu sana, mlifanya maamuzi sahihi kuchagua mbunge huyu. Naomba tumuunge mkono, tusimkatishe tamaa, tumtie moyo na tumuunge mkono kwa kumpa ushirikiano, huyu ni mtoto wetu tusitafute mtoto mwingine,"amesema RC Senyamule.
Akitoa salamu zake Anthony Mavunde amesema kuwa lengo la kugawa mitungi hiyo ni katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi kutumia gesi na nishati mbadala na kuacha kutumia mkaa na kuni ili kuepukana na uharibifu wa mazingira nchini na anamini mitungi hiyo itaendelea kulinda mazingira.