Ijumaa , 13th Mar , 2015

Ligi ya Mpira wa Wavu ya Mkoa wa Dar es salaam inatarajia kuendelea kutimua vumbi hapo kesho Uwanja wa Shule ya Uhuru, Jijini Dar es salaam kwa kuzikutanisha timu za Tanzania Prisons na JKT huku Polisi Marine wakicheza na Twalipo.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es salaam DAREVA, Siraju Mwasha amesema, michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwisho wa wiki ambapo siku ya Jumnapili itazikutanisha Timu za Jkt na Makongo huku Jeshi Stars wakimaliza na Tanzania Prisons.

Mwasha amesema, mashindano hayo yenye lengo la kukuza vipaji na kutafuta vipaji vipya yanashirikisha timu nane za wanaume na nane za wanawake kutoka mkoa wa Dar es salaam ambapo kwa wiki hii zitacheza timu za wanaume.

Mwasha amesema, mashindano hayo yanayotarajiwa kumalizika Agosti mwaka huu, yamekuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu shiriki kuwa na muda mrefu wa kufanya maandalizi.