Jumatano , 18th Sep , 2024

Mwili wa mtoto Rwegasila Jackson (14) aliyekuwa mkazi wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera aliyezama kwenye maji ya Ziwa Victoria wakati akiogelea na wenzake kwenye fukwe za Gymkana umeopolewa leo.

Wakizungumza na EATV wavuvi walioona mwili huo ukielea kwenye fukwe za mwalo wa Bunena wamesema kuwa walianza kuhisi harufu ambapo waliposogea karibu walikuta ni mwili wa binadamu na kutoa taarifa.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kagera pamoja na viongozi wa eneo hilo wametoa wito kwa jamii kushirikiana kuzuia watoto kuogelea maeneo hatarishi ili kuepukana na matukio ya aina hiyo.