Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka
Agizo hilo amelitoa wakati akijibu kero za wananchi katika Kijiji cha Rukuba ambapo amesema hakuna sheria inayoruhusu mtu kumfanyia ukatili mkewe ama mwanamke kumfanyia ukatili mumewe.
Nao baadhi ya wananchi wakazungumzia ukatili uliopo kwa wanawake ambao wamekuwa wakipitia kipigo na jamii hiyo kuchukuliwa ukatili huo kama jambo la kaida.
"Mabinti wetu wamekuwa wakipitia ukatili wa kipigo kutoka kwa wanaume inafikia wakati hata mwanamke ukitongozwa ukakataa unapigwa na wanaume wa hapa kisiwani" wameeleza