Jumatano , 4th Sep , 2024

Kwanza kabisa muandishi wa andiko hili anakiri wazi hakuna njia sahihi ambayo imewekwa ya kutambua mwanamke sahihi kwa ajili ya maisha yako.

Wengi tunaishi na ule msemo unaosema kosea kujenga ukuta utaweza kubomoa na kujenga upya. lakini siyo mwanamke wa kuoa.

 

1. Mwanamke mchapakazi (anayefanyakazi yaani wote mnaenda kazini asubuhi)
Lazima ukubaliane na ukweli kwamba hawezi kuhudumia nyumba muda wote, sababu kubwa ikiwa ni u-busy wa kazi

2. Mwanamke wa kulea familia na kubaki nyumbani
Lazima ukubaliane na ukweli kwamba hatoweza kutengeneza pesa kwenye familia, hivyo jukumu lako ni kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa upande wa uchumi.

3. Mwanamke mnyenyekevu (hii ni ndoto ya wanaume wengi)
Basi lazima tukubaliane kwamba atakutegemea wewe kwenye kila kitu ambacho kinamuhusu, kuanzia kucha mpaka mjomba kameza shoka.

4. Mwanamke mwenye akili (kwa maana ya uwezo mkubwa wa kupambanua mambo)
Hapa baadhi ya wanaume wanapingana napo sababu hawapendi mwanamke anayejua sana, Kwa hiyo hapa lazima ukubali ukweli ya kwamba itakuwa ngumu kwako kuwasilisha misimamo yako kwake.

5. Mwanamke mzuri (Ijapo kuwa uzuri wa mtu upo machoni pa mtu)
kwenye hili lazima tukubaliane kwamba kuna gharama zake, kuanzia kucha mpaka nywele mpya. (Kumkuta yeye ni mzuri ni suala moja kumfanya aendelee kuwa mzuri ni suala la pili na ndipo kwenye mtihani, kwa sauti ya Shneida Infos wanawake wanapenda hela sana)

Hakuna mwanamke mwenye sifa na vigezo vyote uvitakavyo, ila kila mwanamke anasifa zake ambazo zinamfanya kuwa tofauti na wengine.