Jumatano , 28th Aug , 2024

Aliyekuwa mlinzi wa timu ya Nacional ya Uruguay Juan Izquierdo amefariki dunia leo Agosti 28-2024 akiwa hospitali alipokuwa anapatiwa matibabu baada ya kudondoka uwanjani mnamo Agosti 22-2024 kwenye mchezo wa michuano ya Copa Libertadores dhidi ya Sao Paulo ya Brazil.

(Nyota Juan Izquierdo enzi za uhai wake)

Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X wa klabu ya Nacional imesema “kwa masikitiko makubwa yenye kuumiza mioyo yetu,klabu ya Nacional inatangaza kifo cha mchezaji wetu mpendwa Juan Izquierdo,tunatoa pole nyingi kwa familia,marafiki,ndugu na jamaa, nasi klabu tupo kwenye majonzi na kuombeleza ndani ya kipindi hiki”

Juan Izquierdo aliyekuwa na umri wa miaka 27 aliingia uwanjani  kipindi cha pili  kuchukua nafasi ya mlinzi wa zamani wa Liverpool  Sebastian Coates huku alidondoka mnamo dakika ya 84 bila kugusana  na mchezaji mwenzake  kabla ya kuanza kupatiwa  matibabu ndani ya uwanja baada ya kudondoka uwanjani kwa tatizo la Moyo.