Jumatatu , 26th Aug , 2024

Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Cole Palmer ameanza vyema msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kuhusika kwenye magoli 4 kwenye michezo 2 huku akifunga bao 1 na kutoa pasi za magoli mara 3 sawa na mshambuliaji wa Manchester City Erling Braut Halaand ndani ya msimu 2024-25

(Kiungo Mshambuliaji Cole Palmer)

Cole Palmer aliweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyehusika kwenye mabao mengi zaidi kwenye EPL msimu uliopita 2023-24 baada ya kuhusika kwenye mabao 33 huku alifunga mabao 22 na kutoa pasi za usaidizi wa magoli mara 11.

Ilhali kwenye upande wa Fantasy League, Cole Palmer ni mchezaji wa 5 kwa kukusanya alama nyingi msimu huu akiwa na alama 19 tofauti ya alama 5 dhidi ya kinara Mo Salah wa Liverpool mwenye alama 24.