Akizungumza na EATV Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmedy Ally amekiri kuwa mchezaji huyo kuuzwa nchini Algeria huku upande mwingine ameweka wazi kuhusu maendeleo ya golikipa Ayoub Lakred aliyepata majeraha nchini Misri.
''Fredy Michael alikuwa na mkabata na Simba SC hivyo tumemuuza katika klabu hiyo ya nchini Algeria na ndani ya wiki hii tunakwenda kuwatangazia wanasimba ni timu gani ambayo amekwenda''amesema Ahmedy Ally.
Timu ya Simba SC inayoongoza kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara msimu huu,itarajiwa kushuka dimbani Agosti 25 , 2024 dhidi ya Fountain Gate FC katika mchezo utaopigwa majira ya saa 10 jion katika uwanja wa KMC Complex, Mwege , jijini Dar es salaam