Waziri wa Madini Anthony Mavunde
Hayo yamebainishwa leo Agosti 19, 2024 na Waziri wa Madini Anthony Mavunde mkoani Shinyanga katika hafla fupi ya utoaji wa mfano wa hundi ya shilingi bilioni 10 kwa wachimbaji wadogo na wafanyabiashara wa Madini ikiwa ni mkopo kutoka benki.
Waziri Mavunde amesema kuwa mikopo iliyotolewa itasaidia kuikuza na kuiendeleza Sekta ya Madini na hivyo kupelekea kuongeza kwa mchango wa Sekta ya Madini kwenye pato la Taifa na uchumi wa nchi.
Waziri Mavunde ameipongeza Benki hiyo kwa kutoa mkopo wa Bilioni 10 kwa wachimbaji wadogo na watoa huduma na kutumia fursa hiyo kuzitaka benki nyingine pia kuiunga mkono sekta ya madini kupitia utoaji wa mikopo.
Akitoa salamu, Rais Wa Shirikisho la Vyama vya Wachimba Madini Tanzania (FEMATA) Ndg. John Wambura Bina amempongeza Rais Dkt. Samia kwa uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya madini ambao umeanza kuleta tija na kuaminika kwa wachimbaji wadogo kukopesheka kwakuwa sasa kuna mashine za uchorongaji zinazosaidia kupata taarifa za awali za uwepo wa madini na hivyo kuwatoa wachumbaji kwenye kuchimba kwa kubahatisha.