Nyota huyo wa Muingland mwenye umri wa miaka 23 amekamilisha vipimo vya afya na anatarajiwa kujiunga na Foxes kabla ya klabu hizo hazijakutana usiku wa leo kwenye mchezo wao wa kwanza wa EPL 2024-2025 utakaopigwa King Power Stadium
Skipp aliyekulia kwenye akademi ya Spurs amecheza zaidi ya mechi 100 akiwa na klabu hiyo na msimu uliopita mara nyingi amekuwa akitokea benchi chini ya kocha Ange Postecoglou