Liya'u Sa'adu mwenye umri wa miaka 60
Kwa mujibu wa BBC mkazi huyo anajiona kama "mlinzi" kwa watu wengine wengi wasio na makazi ambao wamejiunga naye.
Liya'u Sa'adu (60) mekua akiishi chini ya daraja kwa miaka 30 sasa kutokana na kutomudu hela ya kulipa kodi.
Bwana Sa'adu anawashauri mara nyingi vijana kutoka miji na vijiji vya mbali juu ya jinsi ya kuwa mitaani katika mji wa Lagos, ambako ni rahisi kutumbukia katika uhalifu na madawa ya kulevya.
"Nina umri wa miaka 60 na kuna vijana ambao walikuja hapa miezi michache iliyopita au miaka michache iliyopita. Ninaona ni wajibu wangu kuwaongoza," aliiambia BBC.
"Ni rahisi sana kupoteza njia hapa Lagos, hasa kwa vijana kwa sababu hakuna familia ya kutazama hatua zao."