Alhamisi , 18th Jul , 2024

Mkufunzi wa Yanga SC Miguel Gamondi amesema anategemea kuwa na msimu mgumu zaidi kwenye msimu mpya wa mashindano 2024-25 kutokana na maandalizi ya klabu zingine kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotaraji kuanza Agosti 16-2024

(Kocha Mkuu wa Yanga SC Miguel Gamondi)

“Tuna kikosi kikubwa chenye wachezaji wenye uwezo mkubwa lakini sitaki kusikia kuhusu Galacticos popote duniani timu nzuri ni yenye uwezo uwanjani na sio kwenye majina ya wachezaji na watu wetu wengi wanadhani tutakuwa na msimu mwepesi lakini nategemea kuwa na msimu ujao kuwa mgumu zaidi kutokana na klabu zingine kufanya maandalizi mazuri pamoja na kufanya usajili wa wachezaji wazuri na hili ni maendeleo kwa soka la Tanzania”- amesema Miguel Gamondi-Kocha Mkuu Yanga SC

Kwa upande mwingine,

Kiungo Mshambuliaji wa Yanga SC Stephen Aziz Ki amesema anafurahishwa na ujio wa nyota Clatous Chama kutoka Simba SC na Prince Dube kutoka Azam FC kwani itasaidia kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao.

“Najisikia furaha kucheza na Chama na Dube ambao wamekuwa na misimu bora hapo nyuma ni furaha kuwa nao ndani ya timu moja,ni jambo jema kwa kuwa tutakuwa na muendelezo mzuri wa kucheza vizuri kwa kuwa tunakuwa na wachezaji wengi wazuri ndani ya timu”-amesema Aziz Ki