Jumatano , 17th Jul , 2024

Timu ya Master Rim FC ya Jijini Dar es Salaam imeweka mipango yake bayana ya kutaka kushiriki kwenye Ligi Kuu Tanzania ndani ya misimu 4 inayokuja kutokana na uwekezaji na mipango mikubwa waliyojiwekea kwa hivi sasa.

(Kikosi cha Master Rim kwenye picha ya pamoja)

Akizungumza na EATV,Mmiliki wa timu hiyo Kassim Ahmed amesema kwa sasa wanakamilisha usajili wa ligi Daraja la tatu na baada ya hapo kupigania nafasi ya kushiriki kwenye ligi ya mabingwa wa mikoa,First League,Championship kabla ya kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara.

“malengo yetu ni kucheza Ligi Kuu kutokana na uwekezaji wetu na Kiufundi tutafanikiwa na kufanikisha malengo yetu kwa kuwa tutaongeza wachezaji na kulisuka benchi letu la ufundi ili liwe bora zaidi na kutimiza malengo yetu’’amesema Kassim Ahmed

Master Rim FC ni timu ambayo kwa sasa inakamilisha hatua za mwisho za usajili kushiriki ligi daraja la tatu mkoa kabla ya kusaka tiketi kushiriki ligi ya mabingwa mikoa ili kusaka tiketi ya kushiriki First League msimu 2025-26.