Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan
Akizungumza kwenye Sherehe za Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi zilizofanyika kitaifa mkoani Katavi jana, Rais Samia alisema anatambua pia kilio cha wana-Katavi cha kununuliwa meli kwani atasema neno baada ya kukamilika uundwaji meli alizoahidi maeneo mengine nchini.
“Serikali yangu itafanya kila linalowekana kuhakisha kuwa Bandari ya Karema mbali ya kuwa eneo kiunganishi na mataifa tajwa itaendelea pia kuwa kitovu cha biashara,” alisema na kuongeza anaelewa umuhimu wa eneo hilo kimkakati.
Rais Samia alieza pia sabubu ya kusimamisha shughuli zote uvuvi katika Ziwa Tanganyika kwa muda wa miezi mitatu ili kutoa nafasi kwa samaki kuzaliana kwani walianza kutoweka kwenye ziwa hilo.
“Watalaamu waliona upungufu na kutoweka kwa samaki katika ziwa Tanganyika na hivyo wakakubaliana nchi nyingine wadau wa ziwa hilo kusimamisha shughuli za uvuvi kwa kipindi cha miezi mitatu,” alisema.
Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imefanya uwekezaji mkubwa wa kiasi cha shilingi bilioni 47.6 kuifanya kuwa bandari ya kisasa zaidi kuliko bandari zote zilipo kwenye maziwa Victoria na Nyasa.
Maboresho ya Bandari ya kimkakati ya Karema ulianza mwaka 2019 na kukamilika mwaka 2022 kwa sasa inafanya kazi kwa muda masaa 24 na inafaa vyote vya kisasa.
Kutoka Bandari ya Karema hadi Bandari ya Kalemie nchini DRC ni umbali kilomita 338 na Bandari ya Moba pia DRC ni Kilomita 298.