Bustani ya Mbogambonga
Wakulima ambao wameanza kutekeleza teknolojia ya kilimo cha matone katika eneo la Tengeru Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, wamesema aina hiyo ya kilimo imeweza kutoa matokeo chanya baada kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya nyanya,Karot,Squash na migomba kwa kutumia kiasi kidogo cha maji katika eneo kubwa la Ardhi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Wataalamu wa teknolojia za kilimo kutoka kituo cha mafunzo ya kilimo cha mbongamboga cha Hot Tengeru kwa kushirikiana na Taasisi za TAHA na TAPP wamesema wakatia umefika sasa kwa wakulima kuzipokea teknolojia mpya zitakazowasaidia kuongeza uzalishaji na kipato na hatimaye kujiondolea umasikini.
Zaidi ya wakulima elfu nane nchini wanatajwa kuanza matumizi ya kilimo cha matone ambapo Mkuu wa Chuo cha Hot Tengeru Arusha Juma Shekidele,Mwakilishi kutoka Taasisi ya TAPP Gideon Matonya Pamoja naye Anthony Chamanga afisa kutoka chama cha wakulima wa mbogamboga na matunda nchini TAHA wamesema teknolojia hiyo ya kilimo inaanza kushika kasi nchini.
Hayo yamejiri wakati wa zoezi la maalumu la utoaji Elimu kwa wakulima juu ya matumizi ya tekolojia zinazoweza kuongeza tija katika kilimo lililofanyika katika kituo cha Hot Tengeru ambapo mamia ya wakulima kutoka maeneo mbalimbali wameshiriki huku uhitaji wa mazao ya mbogamboga ukitajwa kuwa mkubwa hivi sasa katika masoko ya ndani na nje ya nchi.