Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
Tangazo hilo la Bw. Blinken limekuja wakati wanajeshi wa Ukraine wakirejea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kufuatia mapigano makali na vikosi vya Urusi.
Urusi imesema vikosi vyake viliteka makazi mengine mawili katika mkoa wa Kharkiv, ambako vikosi vya Urusi vimekuwa vikizidisha mashambulizi yao.
Gavana wa Mkoa Oleh Syniehubov kupitia ukurusa wake wa Telegram ameandika kuwa, Jeshi la Urusi lilishambulia Shevchenkivsky, Wilaya ya kati ya Kharkiv na kujeruhi watu wawili na kuharibu jengo la ghorofa tano.