Picha ya Quavo
Ukumbi huo una uwezo wa kuchukua mashabiki 5700 lakini waliojiotokeza kushuhudia show hiyo ya Quavo walikuwa watu zaidi ya 100 tu.
Taarifa hiyo imeibua muendelezo wa bifu zito linaloendelea kati ya Quavo na Chris Brown, ambapo inasemekana Chris Brown amenunua tiketi za show hiyo ili kumfelisha Quavo.
Tukio kama hilo liliwahi kutokea kwa 50 Cent kununua tiketi za mbele kwenye show ya Ja Rule na kukaa peke yake ili kuonekana show hiyo haikuingiza watu.