![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2024/03/28/ukaguzi.jpg?itok=ImCOWHlp×tamp=1711657001)
Maofisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani wakifanya Ukaguzi wa magari
Kauli hiyo imetolewa na Kamishna msaidizi wa polisi (ACP) Nassoro Sisiwaya, Mkuu wa operesheni kikosi cha usalama barabarani nchini Machi 28, 2024 kwenye ukaguzi wa vyombo hivyo vya moto mkoani Iringa.
ACP Sisiwaya amesema kuwa, sheria haimtaki tu dereva bali pia mmiliki kuhakikisha chombo husika kinakuwa salama kwa watumiaji wengine kabla ya kuingia barabarani.
Kwa upande wake Kaimu mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Iringa, mrakibu msaidizi wa polisi (ASP) Glory Mtui amesisitiza kuwa operesheni hiyo ni endelevu ili kutokomeza ajali mkoani humo lakini pia kujenga uelewa kwa madereva na wamiliki wote wa vyombo hivyo vya moto.