
Sanctus Mtsimbe
Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea, Dar es Salaam.
Ndugu Mtsimbe anatarajia kuzikwa Jumapili hii makaburi ya Mashujaa Kinondoni.
Sanctus ni Mwanzilishi wa group la Consultants, pia alikuwa ndio Rais wa kwanza wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN), hadi anafariki alikuwa ni Country Manager wa Wananchi Group ambao ndio wamiliki wa Zuku, Simba Net na makampuni mengine.
Ndugu Sanctus pia alikuwa mjasiriamali na mmiliki wa makampuni kadhaa binafsi , pia mjumbe wa bodi kwa taasisi kadhaa za umma na binafsi.
Kifo chake kimetokea ikiwa ni mwaka mmoja na miezi kadhaa iliyopita tangu Bwana Mtsimbe alipoondokewa na kijana wake Jason Mtsimbe na yeye jana amefariki dunia