Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa
Aidha amesema treni ikifika mikoa ya Kigoma na Mwanza matumizi ya uhitaji yatakapoongezeka ndipo umeme mwingi utahitajika na tayari upo kwani wameunganishwa na gridi ya Taifa.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 26, 2024, wakati wa uzinduzi wa safari ya majaribio ya treni ya SGR kati ya Dar es Salaam na Morogoro.
"Watu wasiwe na wasiwasi kwamba umeme utazimia njiani, kuna 'transmission' ya kwetu peke yake kutoka gridi ya Taifa na ili treni iweze kusimama kwa ajili ya umeme basi mjue labda nchi nzima hakuna sehemu ya umeme," amesema Kadogosa