
Sukari
Akizungumza baada ya operesheni hiyo, Afisa kutoka Bodi ya Sukari, ambaye ndiyo aliyeongoza oparesheni hiyo, George Gowele, amesema operesheni hiyo ililenga kuwabaini na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaoendelea kukiuka bei elekezi.
Aidha ameongeza kuwa licha ya serikali kufuta ushuru wa kuingiza sukari nchini lakini bado baadhi ya wafanyabishara wameendelea kukiuka bei elekezi iliyopangwa na serikali hivyo kuendelea kusababisha ugumu wa upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa walaji.