
Hayo yamejiri baada ya wananchi hao kufikiwa na nishati ya umeme wa gridi ya taifa kwa mara ya kwanza kupitia Mradi Usambazaji Umeme Vijijini REA.
"Ulivyofika umeme matarajio yetu kutakuwa na biasahara nyingi katika kijiji chetu cha Ikombe maana umeme ndo kila kitu kwa ajili biashara watu watakuwa na saloon" - Imani Makolo, Mkazi wa Ikombe
"Ambacho tutafaidika hapa ikom be baada ya kufikiwa na umeme watoto wataweza kujisomea hata usiku kwani walikuwa wanashindwa kujisomea usiku kufuatana na mwanga tulikuwa hatuna na ndao kitu ambacho tumefurahi sisi wanakijiji cha ikombe na tunaamini watoto wanasoma vizuri" - Esteria Hanji, Mkazi wa Ikombe
"Tuliakuwa tunatumia vibatari au mishumaa na sola kwa hiyo upande wawafunzi ilikuwa changamoto sana kujisomea ilikuwa mpaka mtu akanunulie mishumaa au mafuta ya taa awashe koroboi hali hiyo kunakuwa hakuna tena mwanafaunzi kujiosomea" - Felista Kimbiu, Mwananchi Kijiji cha Ikombe
"Watumishi wenzangu wanafuraha ni siku nyetu kwetu ni siku tumekuwa tunatumia mwanga wa sola ambao si wa uhakikka kwani mmvua ikinyesha muda mrefu kuna kuwa hakuna tena mwanga hivyo kutuletea tabu hasa wakti wa mama kujifungua nyakati za usiku hivyo basi ujio wa umeme tumepata mwarobaini wa tatizo letu" Joshua Katabazi, Mganga Mfawidhi Zahanati ya Ikombe
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya Josephine Manase amewataka wananchi kutunza miundombinu lakini kutumia nishati ya umeme kujieletea maendeleo huku Meneja wa mradi Mustapha Himba akieleza gharamza za mradi.
"Umeme huu uende ukatukomboe ukatusaidie kiuchumi lakini utakwenda kubadilisha taswila ya kijiji chetu cha Ikombe kwa hiyo niwaome tuchangamkie hii fursa lakini pia ulinzi wa mindombinu kwani serikali imetumia gharama kubwea kufikasha umeme katika katika kijiji cha Ikombe" - Josephine Manase, Mkuu Wa Wilaya Kyela
"Katika utelezaji wa mradi kyela tulikuwa na vijiji thelathini na tano na mpaka sasa tumeshawasha vijiji thelathini na tano kwa na hiki tulicho washa laeo niche thelathini na nne hivyo bado kijiji kimoja" Mustapha Himba, Meneja wa mradi REA.