
Rais wa Zanziba na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi baada ya hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni
Dkt. Mwinyi amesema hayo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri wapya aliowateua hivi karibuni viwanja vya Ikulu Zanzibar leo Februari 01, 2024.
Aidha Rais Dkt. Mwinyi amemtaka Waziri wa utalii na mambo ya kale Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga kuweka juhudi kubwa kupanua wigo katika Sekta ya Utalii hususan utalii wa urithi mikutano na michezo.
Vilevile Rais Dkt. Mwinyi amemtaka Waziri mpya wa Wizara ya Uchumi wa Buluu Mhe. Shaaban Ali Othman kuongeza juhudi katika kuzitatua changamoto za wananchi na kukuza vipato vyao pamoja na fursa za mafuta na gesi katika sekta hiyo.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewaagiza Wizara ya ardhi kutatua migogoro ya ardhi.
Rais Dkt. Mwinyi amesema Kujiuzulu kwa Waziri si jambo geni ni njia ya uwajibikaji, ameeleza kuwa wakati una wajibika kujiuzulu lazima kuwa mkweli kama kuna sababu za mgongano wa kimaslahi utangaze na kusema wazi sababu zilizokufanya uwajibike.