Jumanne , 3rd Mar , 2015

Michuano ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara natarajiwa kuendelea kutimua vumbi hapa kesho katika viwanja vitatu tofauti hapa nchini.

Timu ya Jkt Ruvu inatarajia kuwakaribisha maafande wenzao Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya huku timu ya Ruvu Shooting ikiwa Uwanja wa nyumbani Mabatini Mlandizi kuwakaribisha timu ay ndanda Fc.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar wanatarajia kuwakaribisha majirani zao Polisi Morogoro, mechi itakayochezwa Uwanja wa Manungu Turiani Mkoani Morogoro.