Jumatatu , 22nd Jan , 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametoa wimbo kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujiandaa kwa lolote katika kuelekea chaguzi za serikali za mtaa na uchaguzi mkuu wa 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 22, 2024, wakati akihutubia katika mkutano wa saba wa Mkuu wa Majeshi-CDF na Makamanda wa mwaka 2023, ambapo amebainishwa kwamba amewasilisha ombi hilo kwa kuwa chaguzi hizo zitashirikisha vyama vingi vilivyo na nia tofauti na kwamba si rahisi mambo yote kwenda kama yalivyopangwa.

"Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba mwaka huu na mwakani tunaelekea kwenye chaguzi za nchi yetu na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii, mwaka huu tunaanza na chaguzi za serikali za mitaa kwa sababu tuko wengi, ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa kwahiyo ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza," amesema Rais Samia