Ziara hiyo (Epic Tanzania Tour) imeandaliwa na kampuni ya binafsi ya usafiri ya ‘Insider Expeditions’ na Serikali ya Tanzania iliyoidhinishwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Wawili hao watakwepo katika mashindano ya mchezo wa tenisi yatakayoandaliwa na Gosheni Safaris ambapo kutakuwa na mechi ya kihistoria itakayofanyika Serengeti Desemba 15, 2023.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, watalii hao pia watatembelea “Kijiji cha Utamaduni wa Wamasai”, huku ndugu wa McEnroe wakitoa somo la tenisi kwa watoto wa Kimasai.