Tuachane na hayo, siyo ya msingi sana kwa sasa kuzidi hiki ambacho Issa kiriba kutoka Maswa aliomba kufahamishwa baada ya kuona chapisho letu lililohusu namna ambavyo utaweza kutengeneza YouTube channel yako
Baada ya kuona chapisho hilo alipenda kufahamu vigezo vya namna ambavyo ataweza kutengeneza pesa kupitia YouTube channel yake.
Hivi ni baadhi ya vigezo vya muhimu na msingi kwenye kufikia safari ya kuingiza pesa kupitia YouTube channel yako.
- Birthday zaidi ya 18 kwa maana ya umri wa miaka 18 kwani chini ya hapo basi umiliki wa YouTube channel yako utakuwa chini ya mzazi wako, kwa mujibu wa sheria za YouTube.
- Kwa miezi 12 iliyopita lazima uwe umefanikisha kufikisha idadi ya watazamaji wa maudhui yako wasiopungu 4000
- Lazima uwe na wafuasi (subscribers) wasiopungua 1000
- Nchi yako inawatazamaji au watumiaji wa huduma ya YouTube
- Umefuata vigezo na masharti vilivyowekwa na mtandao huo, ikiwa ni pamoja na kujiepusha na kutumia maudhui ya watu wengine.
- Kwa upande wa YouTube shorts pia utaanza kuhesabiwa kama waingiza pesa ikiwa utapata idadi ya watazamaji milion 3 ndani ya siku 90.
- Kujiunganisha na huduma ya ''Google AdSense'' ambayo itakuwezesha kuchagua matangazo ambayo yataonekana kwenye maudhui yako.
Kubwa na muhimu ni kuzingatia maudhui yako iwe kwenye mfumo wa ''Video'' au ''Shorts'''yawe ni yale ambayo uliyatengeneza mwenyewe epuka kurudia na kutumia maudhui ya watu wengine ikiwa kama sehemu ya kuzingatia sheria za mtandao huo.
Nje ya YouTube wenyewe hivi ndivyo ambavyo unaweza kutengeneza pesa kupitia YouTube channel yako.
- Matangazo: Kutokana na ubora na idadi ya watu wanaofuata maudhui yako, unaweza kupata kampuni ambayo itapendezwa kutangaza na wewe. (kuleta matangazo yao)
- Merchandise shelf: kutengeneza bidhaa nyingine zitakazo husiana moja kwa moja na chapa yako mfano vikombe vya EastAfricaTv, Mabegi ya EastAfricaTV na kuwauzia wale watazamaji wako.
- Super Chat & Super Stickers: Hii ni kwa baadhi ya wale watazamaji wako ambao wengependa jumbe zao zionekane juu zaidi pale mtu atakapokuwa akitazama video zako, na hii mtu analipia ''comment'' yake iwe ''pinned''