
Akizungumza kabla ya kuanza mazoezi ya mbinu za medani za kivita na “show off” katika uwanja wa mazoezi jeshi la Polisi kikosi cha Kituliza ghasia FFU Mbeya, Homera amekemea baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati kutumia lugha za matusi kukashfu viongozi wa nchi na wa Jeshi la Polisi kuacha mara moja na kutoa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya RPC Benjamin Kuzaga kutofumbia macho vitendo hivyo
Katika hatua nyingine Homera amepongeza kazi inayofanywa na vikosi vyote vya Jeshi la Polisi ya kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao unakuwepo na wananchi kufanya kazi zao za maendeleo bila bugudha wala wasiwasi wowote
Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Benjamin Kuzaga ameeleza lengo la zoezi hilo “Show Off” kuwa ni kujiweka vizuri na kufanya mapitio ya mazoezi mbalimbali ya mbinu za medani za kivita yaliyokuwa yakifanyika
Aidha, Kamanda Kuzaga ametumia zoezi hilo la “Show Off” lililohusisha vikosi vyote vya Jeshi la Polisi kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya kuzungumza na baadhi ya wananchi kuhusiana na masuala ya ulinzi na usalama katika maeneo yao ya makazi na biashara
Mazoezi ya “Show Off” yamefanyika kwa vikosi vya Jeshi la Polisi kuzunguka Jiji la Mbeya na Mji Mdogo wa Mbalizi kwa magari na kufanya doria za miguu kuonyesha umahiri wa namna ya kuzuia uhalifu na kukabiliana na hali yoyote ya matishio ya uvunjifu wa amani.