
Hayo yamebainishwa na Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo wakati akizungumza na EATV katika shughuli ya uchangiaji wa damu kwa taasisi ya Mtetezi wa mama iliyopo halmashauri ya wilaya ya Geita ambapo amesema mahitaji ya damu ni makubwa katika hospitali hiyo.
“Tunakuwa tukipata wagonjwa wengi sana kabla ya kufika hospitali unakuta ameshapita kwa waganga wa tiba asili sana kwaiyo akija kufika hospitali unakuta ugonjwa umeshafika kwenye hali ambayo sio nzuri kwaiyo inaitajika elimu ya kutosha kuisambaza kwa jamii hii inayotuzunguka,lakin vile vile kwa wamama wajawazito tunapataga wamama wengi wanachelewa kuja kiliniki anakuja kiliniki mimba imeshakuwa kubwa kwaiyo kama damu ipo chini inampa hatari kubwa yeye na mtoto” amesema Shadrack Omega Mganga Mfawidhi Hospitali ya Nzera
Katika hatua nyingine Taasisi ya Mtetezi wa mama Halmashauri ya wilaya ya Geita wamesema baada ya kugundua changamoto hiyo wameanza mkakati wa kuanza kutoa elimu katika jamii ili kuacha tabia ya kukimbilia sehemu ambazo sio rasimi badala yake kuwahi katika vituo vya kutolea huduma za afya.
“Tumeona kuna chanagamoto kwenye jamii yetu kwa mama wajawazito awakimbilii hospitali moja kwa moja badala yake wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji wakati wa kujifungua unakuta anapungukiwa damu anakufa kwaiyo tunazidi kuwaomba ebu mama mjamzito unapopata taarifa za kuwa mjamzito wahi kituo cha afya upate huduma zilizo bora”Elizabeth Chami, Mwenyekiti Taasisi ya Mtetezi wa Mama wilaya ya Geita.
Sambamba na kuchangia damu Taasisi hiyo imefanya usafi maeneo yote ya hospitali ya Nzera.