
Mayai
Hatua hiyo imekuja baada ya uwepo wa picha zinazosambaa mitandaoni iliyoambatana na maneno yasemayo, "Serikali hailali kama alivyo shetani halali!! wanajua kabisa kwa sababu shetani halali kwahiyo kuna mambo mabaya atayatenda tu!! kiwanda cha mayai Goba kwa wachina kimekamatwa sasa hayo mayai yote sijui yametagwa na kuku gani? tusubiri yanayojiri, usikie teknolojia ilivyo hapo ndiyo utakapojua kwanini kila mtu ana kitambi,".
Aidha Wizara imesema kwamba inawatoa hofu wananchi kuwa imefuatilia suala hilo kwa kina na kujiridhisha kuwa tarifa hizo sio za kweli, ni upotoshaji na hivyo kuitaka jamii kuipuuza.
Wizara pia imesema taarifa hizo zimetengenezwa kwa nia ovu ya kuharibu tasnia ya kuku nchini inayokuwa kwa kasi na kwamba katika kufuatilia zaidi, Wizara imebaini kuwa picha hiyo ya mayai mengi iliyotumiwa ilionekana kwenye mitandao ya kijamii mwaka 2016 na haikupigwa hapa nchini.