
Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza jambo na Mkandarasi wa mradi a ujenzi wa vivuko Songoro Marine ambapo atoa maagizo mardi ukamilike kwa wakati.
Amesema hayo leo Jijini mwanza wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko hivyo tisa, ambapo ameelekeza kivuko cha MV Mara kikamilike ifikapo 15 oktoba, mwaka huu ili kitatue changamoto kwa wakazi wa Musoma vijijini.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mwanza Amos Makalla amesema atahakikisha anaweka usimamizi wa kuhakikisha vinakamilika ndani ya muda uliowekwa.
Naye mkandarasi wa mradi huo Songoro Marine, amesema mradi utakamilika ndani ya muda na kwa ufanisi unaotakiwa.