Jumatano , 11th Oct , 2023

Mr PKP Ommy Dimpoz ameanza harakati za kupunguza kilo 10 kwenye mwili wake baada ya kusema ameongezeka uzito mpaka kufikia kilo 80 kutokana na misosi anayokula.

Picha ya Ommy Dimpoz

"Nimeona siku mbili/tatu hizi vyanda vimezidi nikiangalia kilo zangu zipo 80, nataka tupunguze kama kilo 10 halafu tuanze kutengeneza misuli, nataka niwaambie watoto wadogo hii ndio time ya kuanza kuvua shati" amesema Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz ameanza safari hiyo chini ya Denzel Trainer ambaye huwafanyisha mazoezi mastaa kama Alikiba, Kajala, Ray, Chuchu Hans na Rais Mstaafu wa Awamu ya 4 Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.